Juhudi za Kupambana na Unyanyasaji Unajumuisha Nini?


Unyanyasaji uneweza tendeka pahali popote, ikiwemo kazini. Kujifunza ujuzi wa kukabiliana au kuripoti unyanyasaji ndani na nje ya shule ni ujuzi muhimu sana wa maisha. Watu wazima wanaweza kusaidia kwa:
- Kufanya kazi kupunguza unyanyasaji ndani na nje ya shule kupitia kwa ukuzaji na utekelezaji wa sera na elimu
- Kuwafunza wanafunzi ujuzi wa kutambua na kukabiliana na unyanyasaji
- Kukuza ujuzi wa kuwawezesha wanafunzi kuendelea na maisha
- Kujifunza kuripoti unyanyasaji katika shule au jamii
Juhudi za Kupinga Unyanyasaji PA
Ukurasa wa tovuti wa kupinga unyanyasaji wa Idara ya Elimu ya Masuala ya Usalama wa Shule iko na nyenzo za wazazi, waelimishaji, na wataalamu ambao wanahudumia wanafunzi ndani na nje ya mazingira ya shule.
- Laini ya Ushauri ya Kupinga Unyanyasaji
- Ruzuku Zinazolengwa kwa Juhudi za Kupinga Unyanyasaji
- Nyenzo za Kusaidia Juhudi
- Mikutano ya Mtandaoni

Jududi za Kupinga Unyanyasaji Zinawasaidiaje Wanafunzi?
Juhudi za kupinga unyanyasaji zinaweza kuwasaidia wanafunzi:

Kukuza Ujuzi wa Kukabiliana
Wanafunzi wanahitaji kukuza ujuzi wa kukabiliana ili kuunda ufahamu wa kujua wakati ambao wananyanyaswa na hatua za kuchukua baadae.

Kuripoti Unyanyasaji
Wanafunzi wanapaswa kuweza kuzitambua ishara za onyo, haswa katika mtandao wa kijamii, kutoka kwa watu ambao wanaweza kuwa tishio kwao wenyewe au kwa wengine, na kuweza kuwa na ujasiri wa kuripoti unyanyasaji kwa mtu mzima.

Ujuzi wa Kujitetea
Wanafunzi wanahitaji kujua wakati na jinsi ya kujiongelea.

Kuboresha Ujuzi wa Kutangamana na Watu
Wanafunzi wanapaswa kujua jinsi ya kutangamana na watu wengine kwa kupata mambo ambayo wanafanana na kuunda uaminifu na heshima.

NYENZO
Wazazi, wafanyikazi wa shule, na watu wazima wanaojali wako na jukumu la kufanya ili kuzuia unyanyasaji. Bonyeza hapa ili kujua mengi zaidi kuhusu jinsi ya kusaidia.
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
SalamaKusema Kitu ni programu ya kuzuia vurugu kati ya vijana inayoendeshwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Pennslylvania. Programu hii inawafunza vijana na watu wazima jinsi ya kutambua ishara za onyo, haswa katika mitandao ya kijamii, kutoka kwa watu ambao ni tishio kwa wenyewe au kwa watu wengine, na “kusema kitu” KABLA haijachelewa sana.
Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara