Ushiriki wa Familia

Nafuu kwa Familia

Walezi na wanafamilia wanahusishwa na watoto wao wenye ulemavu kila wakati. Hawapati likizo za wikendi, likizo ndefu, au siku zisizo za kazi. Familia hupata furaha na mapambano, haswa na watoto wao, kila pahali wanapokwenda, kwa kila kitu wanachofanya, kila siku na kila saa ya mwaka. Timu za mabadiliko bora na wataalamu wanapaswa kutambua na kuiheshimu nyanja hii. Kwa kuwahimiza familia kuchukua muda wa mapumziko au nafuu kidogo kutoka kwa shinikizo na wasiwasi ambao unawazingira hao na watoto wao unasaidia kudumisha utendakazi wa wadau wote waliohusishwa kwa mchakato wa mabadiliko bora na pia kuwa wa msaada mkubwa kwa wanafunzi.

Nafuu kwa Familia  image

Je, Nafuu Kwa Familia ni Nini?

first images of Je, Nafuu Kwa Familia ni Nini?
second images of Je, Nafuu Kwa Familia ni Nini?

Kuna wakati kwa maisha yetu ambao tunaweza kufaidika na likizo njema. Nafuu kwa familia huwapa wanafamilia wenye wanafunzi wenye ulemavu nafasi ya kuchukua likizo kutoka kwa majukumu ya maisha ya kila siku ndiposa nao pia waweze kufanya kitu cha kuwapumzisha ilhali wakihakikisha kuwa wanafunzi wao wako salama na wanahudumiwa visawa wakiwa mbali. Familia zinahitaji kujua:

  • Ni kivipi nafuu huwa kwa familia? Ni chaguzi gani za nafuu ziko kwa jamii au kutoka kwa mashirika mengine?
  • Ni njia zipi ambazo wanafunzi, familia, na timu zinaweza kufaidika kutoka kwa nafuu ya familia?
  • Ni vikwazo vipi vinazuia familia kujua na kutumia nafuu ya familia? Ni nini inaweza kufanyika ili kuviepuka vikwazo hivyo?
  • Ni kivipi nafasi za nafuu kwa familia zinaweza kutengenezwa kwa familia ndani ya jamii? Ni misaada na ushirikiano upi unaweza kuundwa ili kutoa nafuu hizo kwa familia?
  • Ni jinsi gani habari husambazwa kwa njia tofauti tofauti na kwa muundo ulio wa kirafiki kwa familia? Je, familia wako na njia salama ya kurudisha habari kwa timu kuhusu mahitaji yao?
Video Explainatory Icon

Ushiriki wa Familia: Nafuu kwa Familia

Video Explainatory Arrow

Nafuu kwa Familia Hujumuisha Nini?

Timu ya mabadiliko bora inaweza kuisadia familia iliyo na nafuu au mapumziko kwa kuhakikisha kuwa timu....

  • Inatambua utunzaji salama na wa kimsaada kwa mwanafunzi mwenye ulemavu wakati ambapo familia yake imechukua muda wa mapumziko
  • Kutengeneza njia salama na za kuhamasisha familia kuhudhuria vikundi vya msaada na mikutano za familia na kuwasilisha mawazo na hisia zao
  • Kuwasiliana kuhusu msaada ulioko kwa familia kwa njia iliyo wazi na kwa mbinu tofauti tofauti ambazo zinaheshimu utamaduni, mtazamo, na inayokaribisha kwa wakati wote
  • Hujumuisha wanajamii na mashirika ambayo yanaweza kufikia familia
  • Hauhitaji malipo yoyote kutoka kwa familia ili wafaidike na habari, miunganisho, na nafasi za kutulia na kupunguza msongo wa mawazo kwa familia
Nafuu kwa Familia Hujumuisha Nini?  Image

Ni Nini Nafuu kwa Familia Hutoa?

Wakati ambapo timu ya mabadiliko bora husaidia familia kwa kuipa nafuu, familia itapata...

Huduma ya Kibinafsi  icon

Huduma ya Kibinafsi

Timu hiyo inazitambua na kutoa ujumbe kuhusu nafasi za kupambana na msongo wa mawazo na kutulia, kulingana na mahitaji ya kibinafsi ya familia, bila malipo yoyote kwa familia, na pia kwa mbinu ambayo ni ya kirafiki kwa familia.

Msaada Ulio Salama icon

Msaada Ulio Salama

Timu inahakikisha kuwa familia inajihisi kuwa salama na yule ambaye anatoa nafuu kwa familia na kuwatunza wanafamilia wako mapumzikoni au wakihudhuria mikutano na/au nafasi za kibinafsi au za familia kukua.

Msaada wa Jamii  icon

Msaada wa Jamii

Timu hiyo inawawezesha wanafamilia kuunganishwa na kushirikiana na wanajamii wengine kwa njia iliyo salama na ya kimsaada na kukuza ujuzi wao wa uongozi katika mchakato wa mfumo wa mabadiliko bora.

Nafasi za Mafunzo icon

Nafasi za Mafunzo

Timu inaunda nafasi kwa familia kupata habari kupitia njia ya kukaribisha, iliyo ya kitamaduni mbali mbali, na kwa mbinu tofauti tofauti. Pia familia inapewa nafasi ya kuwasilisha kinachowasumbua, wasiwasi wao, na habari kurudi kwa timu kwa njia iliyo salama na kwa mazingira ya uaminifu.

Career Interested

NYENZO

Unatafuta utunzaji wa nafuu PA?

CHUNGUZA ZAIDI

Latest EVENT DATE

MATUKIO YA HIVI PUNDE

Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.

CHUNGUZA ZAIDI

Want to Learn PA Secondary

Unataka kujifunza zaidi?

Njia ya Umoja ya Pennsylvania iko na habari zaidi za kusaidia kupata programu za nafuu karibu na wewe.

Bonyeza kwa kiungo hiki ili kujifunza mengi.

Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

TOP