Huduma za Mabadiliko Bora ya Kabla ya Ajira


Huduma za Mabadiliko Bora ya Kabla ya Ajira (Pre-ETS) huwasaidia wanafunzi kujifunza kuhusu nafsi zao, kujifunza ujuzi wa kazi, na kuchunguza mafunzo tofauti na kuchagua kazi. Wanafunzi ambao wanahitaji huduma hizi wanaweza kujipeleka wenyewe katika ofisi za OVR zilizo katika wilaya zao. Kikundi cha wanafunzi kinaweza kupelekwa kwa ofisi za OVR na wafanyikazi wa shule wakishirikiana na ofisi ya wilaya ya OVR. Kila mwanafunzi anahitajika kujaza Fomu ya Kupelekwa OVR ya Pre-ETS. Chaguzi za Pre-ETS ni pamoja na:
- Mafundisho ya Kujitetea inawafunza wanafunzi jinsi ya kutatua matatizo na kusimamia maisha zao
- Mafunzo ya Utayari Kazini inawafunza wanafunzi jinsi ya kupata na kuhifadhi kazi.
- Ushauri wa Uchunguzi wa Kazi inawasaidia wanafunzi kujifunza kuhusu kazi na namna ya kuchagua taaluma ya kazi.
- Ushauri wa Mafunzo ya Baada ya Shule ya Sekondari inawasaidia wanafunzi kuchagua iwapo chuo au mafunzo ya baada ya shule ya upili ndio ya manufaa kwao.
- Mafunzo ya Kikazi huunganisha yale wanafunzi wanajifunza shuleni na kazi za kweli huko nje.
Kuwasaidia Wanafunzi Kupata Huduma za OVR
Wakati mwema wa OVR kufungua kesi ni wakati ambapo mwanafunzi ako tayari kujihusisha na shughuli zinazohitajika kutengeneza lengo la ajira linalojumuisha ushindani. Shughuli hizi ni pamoja na utengenezaji wa mpango wa kibinafsi wa ajira (IPE) na kujihusisha kwa huduma za kiufundi ili kuajiriwa. Wakati ambapo hivi hutokea ni wa kipekee kwa kila mwanafunzi. Wanafunzi wanaweza kutuma maombi ya huduma za OVR kwa njia mingi:
- Binafsi ay na mshauri wa OVR
- Kupitia kwa maombi ya awali mtandaoni
- Kujaza fomu ya karatasi ya maombi ya awali

Huduma za OVR Zinawezaje Kuwasaidia Wanafunzi?
Ikiwa timu za mabadiliko bora zitawaunganisha wanafunzi na OVR, wanaweza kupata fursa ka kufikia:

Huduma za Mabadiliko Bora ya Kabla ya Ajira
Huduma za Mabadiliko Bora ya Kabla ya Ajira (Pre-ETS) inaweza kuwasaidia wanafunzi kujifunza kuhusu nafsi zao, kujifunza ujuzi wa kazi, kuchunguza nafasi zilizopo za mafunzo, na kuchagua kazi.

Huduma za Ukarabati wa Kiufundi
Huduma za kibinafsi ambazo zinamsaidia mtu kujitayarisha kwa ajira, kupata ajira, na kutunza ajira.

Wafanyikazi wa OVR
Uwezo wa kuwafikia waratibu wa mapema, washauri na waratibu wa huduma za biashara ili kuwasaidia kutumiza malengo yao ya ajira.

Msaada Maalum wa Ulemavu
OVR iko na huduma maalum kwa viziwi ama watu wenye upungufu kwa kusikia na vipofu au watu wenye upungufu wa kuona.
Nyenzo Zilizoangaziwa
Jumuiya ya PA ya Mabadiliko Bora inatoa nyenzo zinazoangazia maudhui tofauti tofauti, zote zikiwa zinalenga kuboresha matokeo bora kwa wanafunzi wenye ulemavu.

NYENZO
Bonyeza hapa kufikia maombi ya mtandao ya OVR (Bonyeza “ Omba Huduma” kujaza fomu ya maombi ya awali ya OVR)
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Chunguza habari zaidi kuhusu jinsi OVR inaweza kuwasaidia wanafunzi walio katika umri wa mabadiliko bora
Tembelea tovuti ya OVR moja kwa moja.
Angalia Maswali Yote ya Mara kwa Mara