Uzoefu wa Kazi za Kulipwa Zinajumuisha Nini?


watu wazima wanaweza kuwasaidia wanafunzi kujitayarisha kwa Uzoefu wa Kazi ya Kulipwa kwa:
- Kuwasaidia katika uchunguzi wa taaluma ya kazi
- Kujifunza ujuzi wa mahojiano ya kikazi, ujuzi wa kijamii, na ujuzi unaohitajika pahali pa kazi
- Kutoa nafasi ya madarasa yanayofunza ujuzi wa taaluma ya kazi
- Kutoa nafasi za mafunzo yanayolenga kazi maalum
OVR Inawezaje Kuwasaidia Wanafunzi Kupata Uzoefu wa Kazi za Kulipwa?
OVR (Ofisi ya Ukarabati ya Kiufundi) inawasaidia wanafunzi kupata uzoefu wa kazi za kulipwa na kuwapa nafasi za kuchunguza taaluma za kazi na kuelewa hali ya kazi kupitia kwa ufichuzi wa mazingira ya kazi. Ushiriki katika kazi ya kulipwa ni pamoja na nafasi zilizopo wakati wa shule au baada ya shule. Nafasi hizi hutolewa kwa mazingira inayojumuishwa kwa kiwango cha juu iwezekanavyo. Uzoefu wa kazi ya kulipwa iko na faida tele:
- Wanafunzi hupata maarifa na ujuzi wa kuwasaidia kuunganisha shule na shughuli za kazi na nafasi za taaluma ya kazi ya siku za usoni.
- Wanafunzi wanahusishwa moja kwa moja kupitia mwajiri au kujihusisha na jamii.
- Wanafunzi hupata hundi ya malipo kwa kupitia mwajiri au kwa marupurupu.

Uzoefu wa Kazi ya Kulipwa Inawasaidiaje Wanafunzi?
Wakati ambapo mwanafunzi anajihusisha na Ajira ya Kulipwa, atapata:

Uchunguzi wa Taaluma ya Kazi
Wanafunzi wako na nafasi ya kuchunguza taaluma ya kazi kulingana na maazimio yao na mapendeleo yao. Hii inawapa fursa ya kuona kazi ambazo zipo ndiposa watengeneze malengo ya hatua wanazohitaji kufuaata ili kufikia taaluma ya kazi ilhali wakipata malipo.

Ujuzi wa Taaluma ya Kazi
Kwa kufanya kazi pamoja na rika zao na wataalamu, wanafunzi wanaweza kukuza ujuzi wao wa kutangamana na jamii, ujuzi wa mahojiano ya kikazi, na ujuzi wa usimamiaji unaohitajika kwa kazi za siku za usoni.

Nafasi za Kuunda Mitandao ya Watu Muhimu
Kuunganishwa na marika, walimu, na wataalamu unawapa fursa wanafunzi kutengeneza miunganisho na watu ambao wanaweza kuwasaidia kuajiriwa kwa kazi ya juu siku za usoni.

Kazi za Juu
Kupata na kuhifadhi kazi inawapa wanafunzi nafasi ya kujifunza na kuongeza ujuzi wa kazi. Hii inaweza kuwaelekeza kwa kupata kazi za juu au kusonga mbele kikazi.
Nyenzo Zilizoangaziwa
Jumuiya ya PA ya Mabadiliko Bora inatoa nyenzo zinazoangazia maudhui tofauti tofauti, zote zikiwa zinalenga kuboresha matokeo bora kwa wanafunzi wenye ulemavu.

NYENZO
Tazama nyenzo za kukuza taaluma ya kazi kutoka kwa Idara ya Elimu ya PA.
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Tazama Utayari wa Taaluma ya Kazi ya PA!
Jifunze mengi kuhusu jinsi wanafunzi watajifunza kuwa na ushiriki wa maana katika masomo ya baada ya shule, mafunzo ya kazini, njia za taaluma ya kazi, na kama wananchi waliowajibika na kuhusishwa.
Angalia Maswali Yote ya Mara kwa Mara