Kufanya Mipango ya Maisha ya Baadaye


Ili kupanga maisha ya siku za baadaye, timu za mabadiliko bora zinaweza kuwafunza wanafunzi:
- Jinsi ya kuomba msaada, kufanya maamuzi, na kutatua matatizo
- Ujuzi wa kuishi maisha ya kujitegemea kama kusimamia afya na dawa, na kuwa salama nyumbani
- Njia za bajeti, kutunza pesa, na kutumia benki
- Jinsi ya kuchambua nafasi za kuishi kwa kuzingatia pahali ambapo wangetaka kuishi
Kupanga Mipango ya Maisha ya Baadaye
Timu za mabadiliko bora zinapaswa kuwasaidia wanafunzi kujiandaa kwa maisha ya wakati ujao kwa kutathmini na kutoa maelezo katika sehemu zifuatazo:
- Mawasiliano
- Ujuzi wa kutangamana na watu
- Kujitetea na kujiamulia
- Ujuzi wa maisha ya kila siku
- Afya
- Ushiriki wa jamii
- Burudani
- Usafiri

Kupanga Mpango wa Maisha ya Baadaye Unawezaje Kuwasaidia Wanafunzi?

Ujuzi wa Mawasiliano na Kutangamana na Watu
Ujuzi wa mawasiliano unjamuisha uwezo wa kupeana maelezo kamili, kuwasilisha mawazo, na kuweza kuhakikisha kuwa mawasiliano yameptishwa kwa njia ambayo watu wengine wanaweza kuelewa. Ujuzi wa kutangamana na watu ni uwezo wa kuwasiliana na kushirikiana na watu wengine.

Kujitetea na Kujiamulia
Kujitetea ni uwezo wa kuongea na kuomba majumuisho yanayokuzingatia ipasavyo. Kujiamulia ni kujua na kujiamini na kutumia nyenzo bora ili kuhakikisha matakwa na mahitaji yametimizwa.

Ujuzi wa Afya na Maisha ya Kila Siku
Ujuzi wa afya na maisha ya kila siku inajumuisha kujua usafi wa kibinafsi, jinsi ya kutumia mbinu tofauti za usafiri, na jinsi ya kutangamana na watu wengine na kuweza kujitetea. Injumuisha pia uwezo wa kufanya shughuli za kawaida za kila siku na kuzitumia rasilimali ya jamii kwa ufanisi.

Burudani, Ushiriki wa Jamii, na Usafiri
Ushiriki wa jamii ni kuhusishwa katika maisha ya jamii kama ununuzi katika maduka ya mtaa, kujiunga na vilabu au vikundi, kujitolea kwa shughuli za jamii, na kuzuru daktari, na pia kushiriki katika burudani. Kujifunza ujuzi wa kusafiri kwa kujitegemea na kwa usalama katika jamii itajumuisha kuielewa usafiri wa umma, kujifunza jinsi ya kuendesha gari, na kuifahamu mazingira ya jamii.

NYENZO
Mada ya Video: Maisha ya Kujitegemea ( Kituo cha Kitaifa cha Wazazi cha PACER kwa Mabadiliko Bora na Ajira
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Nimejiamulia!
Tazama nyenzo hii bora kwa Nimejiamulia:
Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara