Kupata Maarifa, Kuweka Malengo


Timu ya mabadiliko bora imewekezwa na kuwasaidia wanafunzi kuzijua nafasi zilizopo baada ya shule ya upili na nafasi za mafunzo na kuwasiadia kutambua mvuto wao, mapendeleo yao, na ushupavo wao unaohusiana na masomo na mafunzo zilizopo baada ya shule ya upili. Kwa kutumia mbinu za ki-umri za kutathmini uhali wa mwanafunzi, timu hii inaweza kumsaidia mwanafunzi kuanza kujiuliza maswali muhimu na kuweka malengo yanayokusudia masomo au mafunzo ya usoni. Utathmini unafaa kusaidia kujibu maswali kama haya:
- Wanafunzi wanapendelea au kufaulu kwa masomo au kozi aina gani wakiwa shule ya upili?
- Wanafunzi wana malengo gani ya taaluma na kikazi?
- Ni masomo au mafunzo gani yanahitajika kupata ajira kwa taalluma ama kazi hizo?
- Ni ujuzi upi unahitajika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafaulu kwa mazingira ya masomo ya baada ya shule ama mafunzo?
Watu Wazima Wanawezaje Kuwasaidia Wanafunzi?
Timu ya mabadiliko bora inaweza kuwasaidia kupanga masomo na mafunzo ya baada ya shule ya upili kupitia mbinu zifuatazo:
- Kuwasaidia wanafunzi kuzitambua nafasi zilizopo za masomo na mafunzo baada ya kuhitimu na pia vile vile kuhakikisha kuwa nafasi hizo zinaambatana na ushupavo na mvuto wa wanafunzi.
- Kuhakikisha kuwa mipangilio na ratiba za wanafunzi zinawapa nafasi ya kujihusisha kwa madarasa na mafunzo yanayolingana na masomo au mafunzo waliyotambua.
- Kuwapa wanafunzi mafunzo ya moja-kwa-moja na pia kuwapa nafasi ya kuendeleza ujuzi utakaowasaidia kufaulu katika masomo au mafunzo waliochagua. Hii inahusisha kuwasadia kujaza fomu za maombi ya chuo na pia kujifunza ujuzi wa mahojiano.
- Kuwaunganisha wanafunzi na wafanyikazi kwa taaluma za kazi wanazozipenda ili wajue mahitaji muhimu za mafunzo zinazohitajika kufaulu katika kazi wanazowania kufanya usoni.

Mipangalio ya Baada ya Shule ya Upili na Chuo: Njia ya Kufaulu
Timu za mabadiliko bora zinaweza kuwasaidia wanfanuzi kujiandaa kufaulu kwa masomo na mafunzo ya baada ya shule ya upili kwa kupitia njia sahihi ya kufaulu.

Weka Mpangilio
Kuweka mpango wazi ambao unaunganisha uwezo wa ushupavu, maazimio, na malengo ya kikazi ya wanafunzi na nafasi za masomo na mafunzo zilizopo baada ya shule ya upili.

Kukidhi Masharti
Kuhakikisha kuwa wanafunzi wamekidhi masharti yote ya kozi wanazotaka kufanya baada ya shule ya upili. Pia kuhakikisha kuwa wamepata maarifa na ujuzi unaohitajika kujiunga na masomo au mafunzo ya baada ya shule ambayo inaambatana na malengo yao ya kikazi.

Kujenga Ujuzi wa Baada ya Shule ya Upili
Kuwatayarisha wanafunzi kwa kujenga ujuzi ambao wanahitaji kufaulu kwa masomo na mafunzo ya baada ya shule ya upili, ikiwemo jinsi ya kutunza saa, kujipanga vyema, na kujua kuweka vipaumbele.

Kujifunza Ujuzi wa Taaluma ya Kazi
Kuwaelekeza wanafunzi kuzijua ujuzi amabazo zinahitajika ili kupata kazi wanazotaka na pia kufaulu katika njia ya kazi wanayochukua kwa kutumia ujuzi huo.
Nyenzo Zilizoangaziwa
Jumuiya ya PA ya Mabadiliko Bora inatoa nyenzo zinazoangazia maudhui tofauti tofauti, zote zikiwa zinalenga kuboresha matokeo bora kwa wanafunzi wenye ulemavu.

NYENZO
Je, unataka kujifunza mengi kuhusu chuo na masomo ya kazi kwa PA?
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayoweza kukufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka Kujifunza Zaidi?
Angalia hii karatasi ya kuweli inayatoa ujumbe wa kuwasaidia wanafunzi kujua nini kinachowasibiri katika masomo ya baada ya shule ya upili.
Wanafunzi wanapojua cha kutarajia baada ya shule, inawapa fursa ya kujiandaa vyema kufaulu katika masomo na mafunzo.
Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara