Kwanini Wanafunzi Wanapaswa Kushiriki Katika Programu Ya Kabla Ya Chuo?


Kunazo faida nyingi kwa wanafunzi kushirikia katika programu ya kabla ya chuo.
- Wanafunzi watapata fursa ya ‘kujaribu’ chuo. Hii itawasaidia kuangazia maeneo ya uwezo na maeneo ambayo yanahitaji uboreshaji.
- Programu ya kabla ya chuo ni zaidia ya ziara. Wanafunzi wanaweza kuhudhiria madarasa, kuishi chuoni, na kufurahia yale ambayo chuo inatoa.
- Wanafunzi wanaweza kuhudhuria madarasa ya chuo wakati wa likizo ndefu
Je, timu za mabadiliko bora zinawezaje kutoa msaada wa ufikiaji wa programu za kabla ya chuo?
Kufikiria kuhusu chuo inaweza kuwapa familia wasiwasi wa moyo, lakini yule anayeptia shida zaidi ni wanafunzi. Hizi ni mbinu kadhaa ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi kuamua kama chuo inawafaa.
- Kagua maazimio, uwezo, na maeneo ya uboreshaji
- Chunguza vyuo mtandaoni
- Wasaidie wanafunzi kwa kuwauliza maswali kama; je, hii chuo inatoa nafasi ya uzoefu wa kabla ya chuo? Ni vipi mtu anaweza kufikia ofisi ya ulemavu kutafuta msaada?

Kwanini Uhudhurie Programu ya Kabla ya Chuo?
Faida za kuhudhuria programu ya kabla ya chuo ni pamoja na:

Maarifa ya Programu
Wanafunzi watajifunza kuhusu programu zilizopo kwa ajili yao na jinsi ya kutuma maombi ya kujiunga nazo.

Maarifa ya Msaada
Wanafunzi watazigundua misaada ya masomo na maisha ya kujitegemea ambayo inapatikana katika chuo au chuo kikuu.

Alama za Chuo
Wanafunzi wanaweza kupata alama za kutumika chuoni kwa kozi wanayohudhuria ilhali bado wakiwa shule ya upili.

Ujuzi wa Chuo
Wanafunzi watajifunza kwa kikweli kuhusu maisha ya kuishi katika chuo.

NYENZO
Seti ya zana ya Masomo na Mafunzo ya Baada ya Shule Ya Sekondari ya NTACT inatoa nyenzo za kutoa usaidizi wa kufikia na kufaulu katika Masomo na Mafunzo Ya Baada Ya Shule Ya Sekondari
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Chuo cha Kufikiri cha PA
Chuo cha Kufikiri ni ushirikiano wa vituo vya elimu ya juu ambazo zimejotolea kubuni na kusaidia mazingira ya chuo ili kuwezesha masomo ya ujumuishaji kwa vijana wenye ulemavu wa kiakili.
CHUNGUZA ZAIDI