Jukumu la Timu ya Mabadiliko Bora kwa Kuwatayarisha Wanafunzi kwa Kazi ya Likizo


Timu ya mabadiliko bora inapaswa kuwasaidia wanafunzi kufanya uchunguzi wa jinsi ajira za likizo zinatekelezwa. Hii ni pamoja na:
- Kuzungumza na wanafunzi kuhusu maazimio yao, uwezo wao, mahitaji yao, na mapendeleo yao ya kikazi
- Kuwasaidia wanafunzi kufanya uchunguzi wa programu za likizo na kazi ambazo ziko katika jamii
- Kujaza fomu tofauti za kazi za likizo na kujifunza mbinu za kujibu maswali ya mahojiano ya kazi
- Kutambua mahitaji ya usafiri ya wanafunzi ya kwenda na kurudi kutoka kwa shughuli za kazi ya likizo
Ofisi ya Ukarabati ya Kiufundi (OVR) ya Kazi za Likizo
OVR iko na uhusiano na waajiri walioko katika jamii wa kuwasaidia wanafunzi kupata uzoefu wa kazi wakati wa likizo. Kazi za wakati wa likizo ndefu kwa kawaida hudumu kwa wiki tano hadi saba na huwasaidia wanafunzi ambao wangekuwa na wakati mgumu wa kupata kazi. Programu za kazi za wakati wa likizo hutoa:
- Marupurupu au malipo
- Uzoefu wa kazi iliyopangwa katika jamii
- Msaada kutoka kwa mratibu wa mafunzo aliye katika mazingira ya kazi

Uzoefu wa Ajira za Wakati wa Likizo Zinawasaidia Wanafunzi Kivipi?
Ajira za wakati wa likizo hutoa fursa bora ya kutengeneza uhusiano na watu tofauti, kuendeleza ujuzi wa kutangamana na watu katika jamii, na kuboresha ujuzi wa taaluma ya kazi.

Ujuzi wa Taaluma ya Kazi
Wanafunzi wanaweza kujifunza ujuzi kama kutengeneza vyeti vya kutafuta ajira, kujaza fomu ya kufanya maombi ya kazi, ujuzi wa mahojiano ya kutafuta kazi, na kusimamia majukumu kazini.

Ujuzi wa Kutangamana na Watu
Wanafunzi hupewa nafasi ya kutangamana na rika zao na wafanyikazi wenza ili kujua mbinu za kujadiliano kwa mazungumzo ngumu na wengine. Vile vile, hao hujifunza kuwa washiriki wa timu katika mazingira ya kazi.

Kuunda Mitandao na Watu
Wanafunzi hutengeneza uhusiano na watu katika mazingira ya kitaaluma. Maarifa na uzoefu wa wataalamu hawa unaweza kuwasaidia wanafunzi katika kutafuta ajira siku za usoni.

Ajira ya Kulipwa
“Uzoefu wa Kujifunza Katika Mazingira ya Kazi imedhibitishwa kuwa mojawapo ya viashiria vya ufanisi katika ajira ya utu uzima kwa wanafunzi na vijana wenye ulemavu.” – Ushirikiano wa Kitaifa wa Utendakazi na Ulemavu kwa Vijana

NYENZO
Bonyeza hapa kujifunza mengi kuhusu OVR
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Tembelea Kiungo cha Taaluma ya Kazi ya PA
Fungua akaunti ya Kiungo Cha Taaluma ya Kazi ya PA ili kupata vifaa vya kutengeneza vyeti vya kutafuta kazi, arifa ya kazi mpya, vifaa vya kufuatilia kazi, na mengi zaidi
Angalia Maswali Yote ya Mara kwa Mara