Jinsi Mchakato wa Ugunduzi Unafanyikaje


Kupitia mchakato wa ugunduzi, timu ya mabadiliko bora hutambua uwezo, maazimio, talanta, na hamu za mwanafunzi kisha wanazitafsiri habari hizo na kuzilinganisha na kazi ambazo mwanafunzi anaweza kufanya ili kufaulu, na mchango anaoleta kwa mwajiri. Mchakato wa ugunduzi unaweza kutumika kama mtihani wa kutathmini huduma za ajira zinazopewa msaada. Mchakato wa Ugunduzi unahakikisha kuwa:
- Wanafunzi wako na fursa ya kutoa ujumbe kuhusu malengo, uwezo, na mahitaji yao.
- Wazazi wako na fursa ya kutoa ujumbe kuhusu kile kiachomweleza mwanafunzi wao vyema na kile ambacho mwanafunzi hufanya vyema.
- Watu wengine pia wanaomfahamu mwanafunzi vyema wako na fursa ya kutoa habari kuhusu kile ambacho mwanafunzi anafanya vyema na nafasi za kujifunza.
Ajira Iliyoboreshwa
Ajira iliyoboreshwa iko na msingi katika uhusiano wa kujadiliana na waajiri badala ya mbinu za jadi za kutafuta kazi. Nafasi ya ajira hutolewa wakati ambapo uwezo, ujuzi, na hali ya ufanisi ya mwanafunzi huambatana na mahitaji ya biashara ambayo hayajatimizwa. Ajira Iliyoboreshwa hutoa:
- Utengenezaji wa wasifu (makaratasi za kazi) za kuona ili kutumia na waajiri
- Kutambua mahusiano ambayo yanaweza kuwepo katika duara la usaidizi wa mwanafunzi
- Ziara na ukaguzi wa mazingira ya kazi ili kuzitazama hali ya kazi na nafasi zilizopo

Ni Nini Mchakato wa Ugunduzi Unaweza Kuwafanyia Wanafunzi?
Wakati timu za mabadiliko bora huwafahama wanafunzi vyema kutoka kwa watu wanaowatambua vyema, mwanafunzi atakuwa na:

Mpango wa Kazi
Mwanafunzi atakuwa na mpango ulio na misaada yote atakayohitaji ili kufaulu katika ajira.

Mpango Uliobinafsishwa
Mwanafunzi atatengeneza mpango wa ajira unaozingatia uwezo, maazimio, na mahitaji yake ya nje ya shule.

Uamuzi wa Kibinafsi
Mwanafunzi atajifunza kuhusu ujuzi wa nyumbani, kazini, na mazingira ya kijamii na anaweza kuweka mipango ya kuboresha ujuzi na kufikia malengo mapya.

Programu Iliyobinafsishwa
Mwanafunzi atafahamisha timu ya mabadiliko bora kuhusu ujuzi na uwezo alionao ili programu ya madarasa zitengenezwe kuzikimu na kuhimiza ujuzi huo.

NYENZO
Bonyeza hapa kwa habari zaidi kuhusu Ungunduzi!
CHUNGUZA ZAIDI

Matukio Yajayo
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Tazama Sera za Ofisi ya Ajira ya Ulemavu
Jifunze jinsi ya kuunda uzoefu wa ajira ulioboreshwa.
Angalia Maswali Yote ya Mara kwa Mara