Ni Nini Timu za Mabadiliko Bora Zinaweza Kufanya ili Kuwasaidia Wanafunzi Kuunda Ushirikiano na Vyuo Vikuu?


Timu ya mabadiliko bora inaweza kusaidia wanafunzi:
- Kuchunguza programu ambazo zinaambatana na malengo yao ya ajira
- Kupanga ratiba ya kuzuru chuo kikuu mtandaoni na kuzuru mwenyewe kimwili
- Kuwaunganisha wanafunzi na ofisi zinazotoa huduma za walemavu
- Kagua vigezo vya kuingia chuo kikuu
- Kukusanya ujumbe unaohitajika kuwasilisha fomu za maombi
- Fanya uchunguzi wa chaguzi ambazo zinaelekeza kwa kupata alama za chuo bado ukiwa shule ya upili
Je, Unajua OVR Inawezatoa Msaada?
Ofisi ya Ukarabati wa Kiufundi (OVR) iko na nafasi nyingi za kuwasaidia wanafunzi katika safari zao za chuo au chuo kikuu. Hizi ndizo baadhi ya nafasi za usaidizi ambazo zipo:
- Ushauri wa uchaguzi wa baada ya shule ya upili kupitia kwa Huduma za Mabadiliko Bora ya Kabla ya Kazi
- Kukuza Programu ya Mafinikio ya Masomo
- Chuo za Likizo za Uchunguzi wa Baada ya Shule ya Upili
- Kituo cha Hiram G. Andrews na Kituo cha Ufundi ya Jumuiya ya Madola
- Nafasi za uwezo wa ufadhili wa elimu ya baada ya shule ya sekondari

Ni Nini Ushirikiano wa Vyuo na Vyuo Vikuu Unaweza Kuwafanyia Wanafunzi?
Kuna faidi nyingi kwa wanafunzi kushirikiana na vyuo na vyuo vikuu wangali bado shule ya upili.

Uchunguzi wa Programu
Wanafunzi watakuwa na nafasi ya kutembelea vyuo vikuu na kutangamana na wafanyikazi na wanafunzi.

Mahitaji ya Kujiunga
Wanafunzi watazifahamu mahitaji yanayohitajika ili kujiunga na programu ya chaguo lao

Huduma za Ulemavu
Wanafunzi wataunganishwa na huduma za ulemavu chuoni ili kujifunza kuhusu vyeti wanavyohitaji na jinsi wataomba shule ili iwazangite kwa ulemavu wao.

Alama za Chuo
Nafasi zingine huwapa wanafunzi fursa ya kupata alama za chuo wakiwa bado shule ya upili.

NYENZO
Tazama habari kuhusu ofisi ya huduma za ulemavu chuoni na mpango wa kuzuru chuo za PA mtandaoni
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Itazame Uandalizi wa Chuo: Mafunzo ya Mtandaoni
Badiliko kutoka shule ya upili hadi chuo ni hatua kubwa kwa kila mtu. Wanafunzi wenye ulemavu wako na mambo mengi ya kuzingatia ukiwalinganisha na wenzao wasio na ulemavu. Tovuti hii huwasaidia wanafunzi katika safari yao ya mazingatio wanayohitaji.
Angalia Maswali Yote ya Mara kwa Mara