Watu Wazima Wanawezaje Kusaidia Katika Uzoefu wa Kazi ya Kutolipwa?


Timu ya mabadiliko bora inaweza kusaidia kutafuta kazi za kutolipwa kupitia:
- Kufanya kazi na wanafunzi ili kuzichunguza nafasi ambazo zipo
- Kumfunza mwanafunzi jinsi ya kufaulu katika mahojiano ya kikazi
- Kumsaidia mwanafunzi kuandika na kusasisha wasifu wake wa kabla na baada ya kila kipindi cha kazi ya kutolipwa
- Kuwa kama washauri na kujihusisha na wanafunzi wakati wa vipindi vya kazi ya kutolipwa
Faida za Mafunzo Kazini Kama Uzoefu wa Kazi ya Kutolipwa
Mafunzo kazini ni nafasi maalum ambapo wanafunzi wanaweza kufanya kazi katika sekta ambazo wanaazimia kuajiriwa siku za usoni. Mafunzo kazini inawapa wanafunzi:
- Ushauri kutoka kwa wataalamu
- Mafunzo halisi ya ulimwengu
- Uzoefu kwa sekta ya maazimio yao
- Nafasi za kutangamana kijamii

Uzoefu wa Kazi ya Kutolipwa Inaweza Kuwasaidia Wanafunzi Kivipi?
Wakati ambapo mwanafunzi anjihusisha na Kazi ya Kutolipwa, atapata:

Uchunguzi wa Taaluma ya Kazi
Nafasi ya mwanafunzi kuchunguza taaluma ya kazi akizingatia maazimio yake na kuzifahamu nafasi za taaluma ya kazi ambazo ako nazo

Ujuzi wa Taaluma ya Kazi
Kukuza ujuzi wa kutangamana na watu, ujuzi wa mahojiano ya kazi, na ujuzi wa usimamizi wa kazi ambao utahitajika na mwanafunzi kwa ajira ya siku za usoni.

Kuunda Mitandao na Watu
Kukutana na watu katika mazingira ya kazi ambao wanaweza kumsaidia mwanafunzi kujifunza kuhusu taaluma ya kazi ya siku za usoni na pia kumsaidia kupata ajira ya kulipwa.

Uzoefu wa Kazi
Kuwa na uzoefu wa kweli wa kazi unaonakiliwa kwa wasifu wa mwanafunzi anapohitimu chuo cha upili.

Nyenzo
Tazama nyenzo za ukuzaji wa taaluma ya kazi kutoka kwa Idara ya Elimu ya PA.
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Tazama Utayari wa Taaluma ya Kazi ya PA!
Jifunze mengi kuhusu jinsi wanafunzi wa PA watajitayarisha kwa ushiriki wa maana katika elimu ya baada ya shule ya upili, katika mafunzo ya kazini, katika njia za kazi, na kama wananchi wanaowajibika na kujihusisha.
Angalia Maswali Yote ya Mara kwa Mara