Uongozi wa Vijana ni Nini?


Uongozi wa vijana unahusisha:
- Kufanya maamuzi
- Kuweka malengo
- Kutatua tatizo
- Kujenga uhusiano
- Mawasiliano
- Kusikiliza
- Kujitambua
- Kuwa na huruma
Ni vipi wanachama wa timu ya mabadiliko bora wanaweza kusaidia kukuza ujuzi wa uongozi kwa wanafunzi?
Wanachama wa timu ya mabadiliko wanaweza kukuza ujuzi wa uongozi wa vijana kwa:
- Kuwafunza kuhusu kujiamini
- Kuwa mfano bora
- Kuweka mipango ya kushirikisha wanafunzi
- Kuwafunza kujipanga vyema
- Kuwahimiza Kuchangia
- Kuwaeleza kuwa kushindwa sio jambo mbaya
- Kuwapa uwezo wa kufanya uamuzi wao wenyewe

Kukuza Ujuzi wa Uongozi Unaweza Kuwasaidiaje Wanafunzi?
Wanafunzi wakipata nafasi ya kuweka vitendoni ujuzi wao wauongozi, watapata:

Kujiamini
Kuamini kuwa wako na uwezo na ujuzi wa kufanya uamuzi muhimu.

Ujuzi wa Kutatua Shida
Kuzitambua changamoto zinazozuia malengo na kuamua suluhu itakayozuia changamoto hizo kabla hazijajitokeza.

Ujuzi wa Maisha
Kutumia mawasiliano ya kufaa, kuwajibika, kuwa na nidhamu, na heshima kwa wengine.

Ujuzi wa Ushirikiano
Kujifunza jinsi ya kufanya kazi vyema na wengine
Nyenzo Zilizoangaziwa
Jumuiya ya PA ya Mabadiliko Bora inatoa nyenzo zinazoangazia maudhui tofauti tofauti, zote zikiwa zinalenga kuboresha matokeo bora kwa wanafunzi wenye ulemavu.

NYENZO
Kituo chaKati cha Atlantika cha ADA– Utetezi wa Vijana na Nyenzo za Uongozi
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI PUNDE
Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka kujifunza zaidi?
Mimi ni Kiongozi PA
Tazama nyenzoya watu wazima na vijana ya kukuza uongozi wa vijana.
Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara