Upangaji Unaoongozwa na Mtu na Familia

Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia

Mwanafunzi anapaswa kuwa kiungo cha kati katika mchakato wa mpangalio wa mabadiliko bora. Muundo wa mpango unaoongozwa na mtu na familia inawaruhusu vijana kuchukua nafasi za mbele za kuchagua programu, huduma, na shughuli ambazo zinaweza kuwasaidia kufikia malengo yao. Hii inajumuisha kuchagua madarasa ambayo wanataka, shughuli ambazo wanataka kujihusisha, na nafasi za nje ya shule ambazo wangetaka kufuata.

Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia  image

Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia

first images of Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia
second images of Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia

Wanafunzi wakishawasilisha maazimio yao, uwezo wao, utu wao, na matamanio yao kwa familia na timu za mabadiliko bora, kinachofuata sasa ni kuchagua programu ambayo itawasaidia wanafunzi kufikia malengo yao ya kazi, masomo zaidi, na kuishi kwa kujitegemea baada ya shule ya upili. Wanafunzi wanapaswa kuwa na chaguzi za programu katika shule na jamii ambazo zinaambatana na malengo yao, uwezo wao, na maazimio yao. Wakati ambapo programu hazimfaidi mwanafunzi, ni haki ya mwanafunzi kuzungumza na timu ya mabadiliko bora kuhusu mabadiliko yanayohitajika. Timu zinapaswa kuzingatia:

  • Mwanafunzi amepewa nafasi ya kujadili na timu ya mabadiliko bora kuhusu masomo, shughuli, ama taaluma za kazi ambazo wanapendelea zaidi?
  • Wanafunzi wamejihusisha kwa programu yoyote ambayo itawasaidia kujitayarisha kwa kazi ya ndoto zao, masomo zaidi baada ya shule ya upili, ama kuishi kwa kujitegemea? Walihisije katika muda huo?
  • Je, wanafunzi wamezungumza na timu za mabadiliko bora kuhusu njia bora za kuboresha programu ili ziambatane na uwezo, malengo, na mahitaji yao?
Video Explainatory Icon

Angalia jinsi wengine wameweka mipangilio kwa kuzitazama video katika tovuti ya ARC!

Video Explainatory Arrow

Je, Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia Unajumuisha nini?

Wadau wa mabadiliko bora wanaweza kuwaisaida wanafunzi kutengeneza mpango unaozingatia mtu binafsi kwa...

  • Kutoa programu na madarasa ndani na nje ya shule ambayo inaambatana na malengo ya usoni ya mwanafunzi, uwezo wa kibinafsi, maazimio, na maadili ya kifamilia
  • Kuwezesha mikutano na mawakili na wataalamu nje ya shule ili kuunda uhusiano na mitandao na watu wengine wanaoweza kusaidia baada ya shule ya upili
  • Kuanzisha mafunzo ya kazi, kazi uvulini mwa mtu au uozefu wowote wa kazi ambao unaambatana na malengo na maazimio ya mwanafunzi
  • Kuwapa wanafunzi chaguzi za shughuli za nje ya shule kama kufuata mambo wanayopendelea na kujitolea ili kukuza ushiriki katika jamii
Je, Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia Unajumuisha nini?  Image

Ni Nini Muundo wa Mpango Unaozingatia Mtu na Familia Unaweza Kukufanyia?

Wakati timu ya mabadiliko bora inapotoa msaada kwa familia, mwanafunzi atakuwa na...

Chaguzi za Kitaaluma ya Masomo icon

Chaguzi za Kitaaluma ya Masomo

Kushiriki katika programu za shule ya upili na baada ya kuhitimu ambazo zinajenga ujuzi wa ajira ya usoni.

Chaguzi za Ajira icon

Chaguzi za Ajira

Kuhusishwa katika kazi tofauti tofauti kabla ya kuhitimu ili wanafunzi waamue uzoefu ambao unaambatana na mbinu zao za kazi na mapendeleo yao. Pia inawasaidia kuchunguza uwezo ambao wanaweza kuwa nazo na hawakuwa wamezitambua awali.

Chaguzi za Kuishi icon

Chaguzi za Kuishi

Kutengeneza mpango ambao utawasaidia wanafunzi kufafanua maana ya “nyumbani” kulingana nao na kuchunguza chaguzi tofauti za kuishi na kujua jinsi ya kutuma maombi ya kuzipata.

Uamuzi wa Kibinafsi  icon

Uamuzi wa Kibinafsi

Kuwasaidia wanafunzi kujifunza kuhusu uwezo wao, mahitaji yao, vipaumbele, na utu wao utawasaidia kuendelea kufanya uchaguzi ambao unawaelekeza kwa malengo yao.

Nyenzo Zilizoangaziwa

Jumuiya ya PA ya Mabadiliko Bora inatoa nyenzo zinazoangazia maudhui tofauti tofauti, zote zikiwa zinalenga kuboresha matokeo bora kwa wanafunzi wenye ulemavu.

Career Interested

NYENZO

Jiunge na Jumuiya ya kujifunza mbinu zinazozingatia mtu binafsi!

CHUNGUZA ZAIDI

Latest EVENT DATE

MATUKIO YA HIVI PUNDE

Tazama kalenda kwa matukio yanayokufaa.

CHUNGUZA ZAIDI

Want to Learn PA Secondary

Unataka kujifunza zaidi?

Chunguza nyenzo hii iliyotengenezwa na Kituo cha Kitaifa cha Elimu ya Shule ya Upili na Mabadiliko Bora

Hii nyenzo inayolenga-mzazi iko na nyenzo za utekelezaji wa mchakato wa upangaji unaozingatia vijana.

Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

TOP