Je, kuwahusisha vijana katika masuala ya mabadiliko bora inajumuisha?


Kutoa nafasi kwa wanafunzi kujihusisha kwa mipangilio ya mabadiliko inawapa sauti kwa maamuzi ya siku zao za usoni. Kuwa na wanafunzi wanaojihusisha na mpango wa mabadiliko unaeza kuwa na mtazamo tofauti kwa kila mwanafunzi. Lakini matokeo mazuri ya baada ya shule ya upili ni sawa kwa kila mwanafunzi.
- Mpango unaompa mwanafunzi kipao mbele
- Mikatuno ya masomo ya kibinafsi inayoongozwa na wanafunzi
- Kushiriki katika kutathmini mabadiliko bora
Wanachama wa timu ya mabadiliko bora wanawezaje kuwasaidia wanafunzi kushiriki zaidi kwa mipangilio ya mabadiliko bora?
Wanachama wa timu ya mabadiliko bora wanaweza kuwashawishi wanafunzi kushiriki zaidi kwa:
- Kuwaelezea mchakato wa Masomo ya Kibinafsi
- Kuwauliza wanafunzi kuhusu habari wanazoweza kufichua na mbinu wanayotaka kufichua habari hizo
- Kuwakubalia wanafunzi kuamua jinsi wanavyotaka kuwa katika mkutano huo
- Kuwasaidia wanafunzi kuchunguza na kuelewa ulemavu wao na pia uwezo wao
- Kufanya matayarisho ya kuigiza kama mbinu ya kujiandaa kwa mkutano na uhusiano na wanafunzi kwa mkutano
- Kukusudia malengo ya wanafunzi, ndoto zao, na nafasi walizo nazo

Je, Mabadiliko Bora Inaweza Kuwasadia Wanafunzi Kivipi?
Faida za kuwahusisha vijana katika mpangilio wa mabadiliko bora ni:

Kuhusika kwa mchakato wa Masomo ya Kibinafsi
Kuelewa mchakato wa Masomo ya Kibinafsi na mabadiliko bora na pia kujifunza kuchukua jukumu muhimu ama kuongoza mikutano ya Masomo ya Kibinafsi.

Kujitambua
Kujihusisha na matayarishi inawasaidia wanafunzi kujitambua vyema. Wanaweza kujua mengi kuhusu uwezo wao, mahitaji zao, utu wao, maazimio yao, maadili yao, na ulemavu wao.

Ujuzi wa Uongozi
Kupata ushupavu wa kuongea na kuifunza tume ya mabadiliko bora kuhusu maisha yao na yale wanayohitaji ili kufikia malengo yao.

Kujiamini
Kujifunza ujuzi wa kulinganisha nafasi tofauti na kuchagua zilizo bora na ambazo zinalingana na uwezo, maazimio, na mahitaji yao ili kupanga jinsi ya kutimiza malengo yao.
Nyenzo Zilizoangaziwa
Jumuiya ya PA ya Mabadiliko Bora inatoa nyenzo zinazoangazia maudhui tofauti tofauti, zote zikiwa zinalenga kuboresha matokeo bora kwa wanafunzi wenye ulemavu.

NYENZO
Nyenzo Zinazozingatia Mpango wa Usoni Unaozingatia Mtu Binafsi, ikiwa imefadhiliwa na ARC
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI KARIBUNI
Tazama kalenda kwa matuko yanayoweza kukufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka Kujifunza Zaidi?
Angalia nyenzo hiiinayoonyesha mkutano wa Masomo ya Kibinafsi iliyoongozwa na mwanafunzi
Angalia Maswali ya Mara kwa Mara ya Mabadiliko Bora ya Secondari ya PA
Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara