Ni nini hufanya majukumu ya watu wazima kuwa ya muhimu?


Watu wazima wenye umuhumi ni wale:
- Wanaaminika na kuheshimiwa na wanafunzi
- Hufuata mbinu ya kibinafsi kuwahudumia wanafunzi
- Huwafikia wanafunzi katika hali zao za kimaisha
- Huwasaidia wanafunzi kuendelea kujielewa zaidi
- Hutambua ndoto, uwezo, na talanta za wanafunzi na pia maeneo wanayohitaji msaada
- Huwahimiza wanafunzi kuamua, kutatua matatizo, na kuhakikisha sauti zao zinasikika
- Huwapatia wanafunzi maoni ya ukweli
Maendeleo ya Vijana, Kuleta Yote Pamoja
Mahusiano ni muhimu! Watu wazima wanaweza kuwasaidia wanafunzi kuleta pamoja maeneo haya sita ya ujuzi:
- Ukuzaji wa Ujuzi wa Kujisamamia
- Ufahamu wa Ulemavu
- Ukuzaji wa Ujuzi wa Kuishi Maisha ya Kujitegemea
- Ukuzaji wa Ujuzi wa Uongozi
- Ukuzaji wa Ujuzi wa Kujiamini
- Kujitambua

Uhusiano wa Watu Wazima Wanaotoa Ushaurikwa Wanafunzi Una Umuhimu Gani?
Wanafunzi wanaweza kusaidika na kufaidika kwa kuwa na uhusiano na watu wazima kwa njia mingi ikiwemo:

Kukuza Mahusiano
Watu wazima wanaweza kuwajulisha wanafunzi kuhusu nafasi zilizopo ambazo zinaambatana na malengo yao ya maisha ya baada ya shule ya upili, ikiwemo taaluma ya kazi na masomo ya chuo.

Kukuza Ujuzi
Watu wazima wanaweza kuwafunza wanafunzi ujuzi wa kimaisha ambao wanahitaji kufaulu kazini, shuleni, na hata nje.

Heshima
Watu wazima wanaweza kuwasaidia wanafunzi kwa kuwajulisha kuwa mawazo yao, malengo yao, maazimio, na maadili zao zinaheshimiwa na watu wazima.

Uaminifu
Watu wazima wanaweza kuwasaidia wanafunzi kukuza uaminifu kwa kuwajulisha kuwa watu wazima huko shule, nyumbani, na kazini wanamakinika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata kile wanachohitaji kufaulu na kujitegemea.
Nyenzo Zilizoangaziwa
Jumuiya ya PA ya Mabadiliko Bora inatoa nyenzo zinazoangazia maudhui tofauti tofauti, zote zikiwa zinalenga kuboresha matokeo bora kwa wanafunzi wenye ulemavu.

NYENZO
Kukuza uhusiano baina ya mwalimu na mwanafunzi
CHUNGUZA ZAIDI

MATUKIO YA HIVI KARIBUNI
Angalia kalenda kwa matukio yanayokufaa.
CHUNGUZA ZAIDI

Unataka Kujifunza Zaidi?
Angalia kijitabu hiki kutoka kwa Muungano wa Mabadiliko Bora ambayo iko na taarifa kuhusu majukumu tofauti katika mchakato wa mabadiliko bora
Mikakati ya Kuunda Msingi wa Kufuatwa kwa Mahusiano
Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara